MAANA,UBORA NA AFYA YA MANII!!
●MAANA,UBORA NA AFYA YA MANII
1.MANII
Ni maji meupe mazito yanayotoka kwa nguvu ya haraka na kumalizika kwa ladha(utamu)
•Manii (Shahawa) kwa kawaida huwa ni maji yanayotokwa kwa mwanamume au mwanamke wakati wa kilele cha raha wakati wa mapenzi.
▪Manii(shahawa) za mwanaume huwa ni mazito na yenye rangi nyeupe
▪Manii ya mwanamke huwa ni mepesi na yana rangi ya njano.
●SIFA ZA MANII YA MWANAUME:
1.Kutoka kwake huambatana na kilele cha raha na kufuatilia uchovu.
2.Harufu yake ni kama chavuo (pollen) ya mtende ambayo huwa kama harufu ya unga uliokandwa.
3.Hutoka kwa kububujika kwa nguvu.
Mojawapo katika sifa hizo inatosha kutambulisha kuwa ni manii.
Ikiwa mtu ametokwa na maji na hazikupatikana sifa hizo basi hayatakuwa ni manii.
●SIFA ZA MANII YA MWANAMKE:
1.Huwa yana harufu kama harufu ya manii ya mwanamume.
2.Kutoka kwake huambatana na hisia ya kilele cha raha na hufuatia uchovu.
▪UTE KILAINISHI(MADHIY)
Madhiy ni maji yenye kunata na yanamtoka mtu aidha anapokuwa anawaza au kutamani kujimai, au hata bila ya kuwaza na hazina sifa kama sifa za manii.Na pia huwatokea wanawake na wanaume ila aghlabu huwatokea sana wanawake.
Inaendelea somo lijalo.
No comments