UMUHIMU WA CALCIUM MWILINI
UMUHIMU/FAIDA YA UWEPO WA MADINI YA CALCIUM MWILINI.
Madini ya Calcium yanayopatikana mwilini ni 2% ya uzito wako.Na 99% yanapatikana kwenye mifupa na meno.
Pia nyingine yanapatikana kwenye (i)Kiini cha neva(nerve cell)
(ii)Damu
(iii)Tishu za mwili (body tissues) na
(iv)Majimaji ya mwilini.
*Calicium(Kalsiamu)
Ni madini yanayosaidia kuimarisha meno na mifupa lakini pia hufanya kazi zingine kama vile:
1.Kusaidia damu kuganda
2.Umeme mwilini (transmission of nerve imulses)
3.Kusaidia misuli kufanya kazi
4.Kuchochea na kutoa homoni(hormones) kama nyongo(Insulin).
5.Husaidia kazi za mfumo wa moyo(Cardiovascular)
Wanawake na Wanaume hukumbwa na tatizo hili la kupoteza wingi wa madini ya kalsiamu mwilini.
Zipo njia tofauti husababisha upotevu huo au mtu kupatwa na ukosefu wa madini haya.
Kwa upande wa
(A)WANAWAKE
(a)Wanawake wanapoteza calcium katika kipindi cha hedhi/bleed
(b)Utumiaji wa sigara
(c)Utumiaji wa pombe kwa wingi
(d)Utumiaji wa kahawa (caffein) na vitu vyenye kaboni(carbon) mfano
Soda hutoa calcium kwa njia ya mkojo.
(B)WANAUME
Hali hizi hazitofauti sana na zile zinazoonekana kwa wanawake isipokuwa suala la hedhi tu.Ijapokuwa zipo njia nyingine zinazoweza kuleta uhaba wa madini haya ya kalsiamu mwilini.
No comments